RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) WAUAGA MWILI WA MFANYAKAZI MWENZAO AMBAYE NI DAKTARI BINGWA WA USINGIZI KWA WATOTO NA WAGONJWA MAHUTUTI ALIYEFARIKI TAREHE 02/05/2018.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mfanyakazi mwenzao ambaye ni Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa aliyefariki tarehe 02/05/2018 jijini Dar es Salaam. Dkt. Onesmo anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 5/5/2018 katika kijiji cha Nzihi kilichopo Iringa vijijini.


Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakielekea katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya kuchukuwa jeneza lenye mwili wa mfanyakazi mwenzao ambaye ni Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa aliyefariki tarehe 02/05/2018.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiimba wimbo wa maombolezo kabla ya kwenda katika chumba cha kuhifadhi maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili kwaajili ya kuchukuwa jeneza lenye mwili wa mfanyakazi mwenzao ambaye ni Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa aliyefariki tarehe 02/05/2018 .

Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani na Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa watoto Godwin Sharau wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) ambao ni marafiki wa karibu wa Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Marehemu Onesmo Mhewa wakieleza jinsi walivyofanya kazi kwa ukaribu na marehemu wakati wa halfa fupi ya kumuaga iliyofanyika leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) lililopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Wafanyakazi wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakiwa na sura za majonzi wakati wa hafla fupi ya kuuaga mwili wa Daktari bingwa wa usingizi kwa watoto na wagonjwa mahututi Onesmo Mhewa iliyofanyika leo katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT) lililopo Hospitali ya Taifa Muhimbili . Dkt. Onesmo anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 5/5/2018 katika kijiji cha Nzihi kilichopo Iringa vijijini.


Comments