RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Balozi Dr. Possi awasilisha hati za utambulisho kwa Papa Francis



Leo May 18, 2018 ningependa uifahamu stori kutoka Vatican ambapo Balozi wa Tanzania, Dr. Abdallah Possi, amewasilisha hati za utambulisho kwa Baba Mtakatifu Papa Francis, Vatican May 17.

Balozi Possi ambaye kituo chake cha kazi ni Ujerumani katika mji wa Berlin pia atahudumia maeneo mengine tisa ya uwakilishi, ikiwemo Vatican.



Kabla ya kuwasilisha hati za utambulisho, Balozi Dr. Possi alipata fursa ya kukutana na viongozi muhimu wa Vaticani, wakiwemo Askofu mkuu, Paul Richard Gallagher, Katibu Mkuu wa Mambo ya Nchi za Nje na ushirikiano wa kimataifa, Askofu Mkuu Angelo Becciu na Katibu Mkuu Msaidizi wa Vatican.

Baada ya uwasilishaji hati, Balozi Dr. Possi alipata fursa ya kukutana na jumuia ya Watanzania waishio Vatican.


Dr. Possi aliwaeleza Watanzania hao kwamba wana jukumu kubwa la kutumia, nafasi zao kuhakikisha nchi ya Tanzania inadumu katika misingi ya uadilifu, umoja na amani ambavyo ni misingi muhimu ya maendeleo.

Comments