RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MHE: BISHOP DR. GERTRUDE RWAKATARE | MAOMBI YA KUONDOKANA NA UMASKINI

BWANA APEWE SIFA.
Binafsi sipendi umaskini, sipendi kutokuwa na pesa, sipendi kuona imani yangu inayumbishwa kwa kukosa pesa, sipendi kudharirshwa eti sina pesa, sipendi kusema vibaya eti unamtumikia Mungu lakini ni maskini. Hakuna anayependa umaskini au kutofanikiwa, kila mtu anapenda kuwa na maisha mazuri na kumtumikia Mungu akiwa na amani ndani ya moyo wake...

Lakini kuna watu wabaya wanaotamani kukuona wewe unabaki chini kiuchumi, unakuwa maskini, unakuwa na maisha ya hofu, unakuwa ni mtu wa kukopa, unakuwa ni mtu wa kutumikishwa eti huna pesa, unakuwa ni mtu ya kukosa chakula ndani ya nyumba yako, unakuwa ni mtu wa kushindwa kusomesha watoto wako wazuri, unakuwa ni mtu wa kukosa hata nauli ya basi, unakuwa ni mtu wa kufanya kazi nyingi lakini kipato hakilingani na unachokifanya..Hii ni mbaya sana na haipendezi.

Mungu hajakuumba ili uteseke KIUCHUMI bali alikuumba ili ufurahie maisha yako huku ukimtumikia. Unajua unapokosa pesa, unaanza kuwa na mawazo mabaya katika kichwa chako, unaweza kufanya vitendo viovu ili upate pesa. 
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Lakini leo ninafunga kila neno baya lililotamkwa usifanikiwe KIUCHUMI, ninaharibu kazi za shetani zinazosababisha ukawa maskini, ninatupa bomo la moto kwa wale waliokunenea mabaya ili usifanikiwe. Ninawakosesha amani popote walipo kwa jina la Yesu. Kuanzia sasa pokea pesa, pokea mafanikio, pokea funguo za mafanikio kwa jina la Yesu. Kama ni mtu wa imani, sema AMEN.

Natamani kuombea kazi ya mikono yako lakini nipo mbali na wewe, ila kwa imani, "Mikono Yako Ikafanikiwe Kwa Kila Jambo utakalofanya siku ya leo kwa jina la Yesu Kristo. Natamani kukushika mkono ila uko mbali, lakini naamini Jumapili hii nitapata nafasi ya kushika mkono wako na kukuombea. Mungu akupe wepesi wa kufika kanisani. Endelea kufanya maombi na ktubu dhambi zako ili Mungu akutakase na kukufungulia milango yako ya mafanikio.

Ninaamini Jumapili hii tutakuwa wote katika ibada zetu hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" ukiwa na ushuhuda. Pia nitaongea na wewe jinsi ya kufanikiwa kupitia kazi ya mikono yako. Natamani kukuona unafurahia maisha ya Kimwili na Kiroho. Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. na Jumatano, Alhamisi na Ijumaa ibada itaanza saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku. Usikose ibada hii na Mungu akubariki sana.

-----------------------
-Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
-Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"
-Kanisa limekuandalia usafiri wa kufika ibadani Jumapili kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.



Comments