RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MHE. BISHOP DR. GERTRUDE : MAOMBI KWA WASIO NA WATOTO

BWANA APEWE SIFA!
Sitamani kukuona una huzunika eti huzai, eti ni tasa, eti ni mgumba, eti mama wa nyumbani. Umesemangwa na mawifi, marafiki, majirani na kila mtu eti wewe mgumba, huzai, tasa na kutajiwa majina ya ajabu ajabu. Inaumiza sana. Ndoa yako imekosa amani, mume wako anakusimanga, hataki hata kukunulia zawadi kama zamani, hatamani hata kulala na wewe, hatamani hata kuongea na wewe, umekuwa ni mtu wa kupigwa, kutupiwa maneno machafu kutoka kwa mumeo na ndugu wa mume wako. Kila ukikaa, una mawazo, unatamani kuachana na mume wako, unatamani kujiua, unatamani kujificha usionekane mbele za watu, unatamani kunywa sumu, unatamani kunywa pombe eti upunguze mawazo. 
Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Mwanangu, nataka nikuambie kuwa yupo Yesu mtenda miujiza, yupo Mungu wa huruma, wapo watumishi wa Mungu wa kulia na wewe!!!. Acha kuwaza mabaya bali waza mema, acha kuamini nguvu za giza bali muamini huyu Yesu atafanya njia pasipo na njia. 

Pengine watu wamekunenea maneno mabaya kwa waganga usizae, pengine bila kujua ulimuacha huyu Mungu na nguvu za giza zikapata nafasi ya kufunga kizazi chako. Siku ya leo sauti ya Mungu inakuita "Njoo nikufute machozi"

Mimi nipo mbali na hapo ulipo kukushika mkono ili nilie na wewe juu ya shida yako. Ila naamuru nguvu za Mungu zikate ugumba huo, ninaamuru nguvu za Mungu ziachie utasa huo, ninaamuru nguvu za Mungu ziwachome na kuwangamiza waliokunenea mabaya ili uzipate watoto. Pokea mtoto wako wa kiume, Pokea mtoto wako wa kike, pokea mapacha kwa jina la Yesu. Kama ni mtu wa IMANI, sema AMEN.

Natamani Jumapili hii nikushike mkono kanisani, tumshukuru Mungu kwa kupokea ujauzito wako kwa iamani, natamani Jumapili hii niguse tumbo lako na kumshukuru Mungu kwa kile kitakachotokea 2018 katika uzao wako kwa imani. Ibada itaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Mungu akupe wepesi wa kupata pesa ili zikusidie kufika kanisani ili niongee na wewe.
-----------------------

-Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
-Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B"
-Kanisa limekuandalia usafiri wa kufika ibadani Jumapili kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola.
=Siku ya Jumatano, Alhamisi na Ijumaa ibada ya maombi itaanza saa 9 alasiri hadi saa 1 usiku.

Comments