RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.03.2018: HAPPY KWAYA NA JOYBRINGERS KWAYA ZA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B" SIKU YA JUMAPILI

TAFAKARI
//MITHALI 12:2. Mtu mwema atapata UPENDELEO kwa BWANA; Bali mtu wa hila atahukumiwa naye.//

Kwahiyo ukitaka Mungu akupendelee katika kazi yako, huduma yako, ndoa yako, familia yako, biashara yako, masomo yako, mipango yako n.k unatakiwa kuwa mwema kwa kutenda yale anayokuagiza kupitia kitabu chake kitakatifu yaani BIBLIA na kuyatii yale unayoaambiwa na watumishi wake walioko hapa duniani kwa kazi yake. 

Watumishi wa Mungu wanaweza kuwa wachungaji, Maaskofu, Wainjilisti, Mitume, Manabii, walimu au waimbaji. Lakini leo tunamshukuru sana Mungu kwa waimbaji wa kwaya ya Joybringers na Happy Kwaya kutoka kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa Neno walilotuachia kupitia nyimbo zao zenye mafuta na upako kutoka kwa Mungu. Uimbaji wao na kucheza kwao kulikonga mioyo ya watu katika ibada ya maombi KUVUNJA ROHO ZA UTASA NA KUTOONGEZEKA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 11.03.2018. Watu walifarijika mioyo yao tayari kwa kusikiliza Neno la Mungu kutoka kwa Mhe. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Wewe uliyekosa bahati hii, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana na siku ya Jumatano na Ijumaa, ibada itaanza saa 9 lasiri hadi saa 1 usiku. Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola jijini dar es Salaam.

Happy Kwaya







 Joybringers Kwaya











Comments