RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

11.03.2018: BAADHI YA WATU WALIOKOKA KATIKA IBADA YA MAOMBI YA KUVUNJA ROHO ZA UTASA NA KUTOONGEZEKA

Siku ya Jumapili 11.03.2018 watu wengi sana waliweza kuokoka katika ibada ya MAOMBI YA KUVUNJA ROHO ZA UTASA NA KUTOONGEZEKA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Mch. Elizabeth Lucas aliwaongoza sala ya toba baada ya hapo jopo la wachungaji waliwaombea na kukemea roho chafu. Waongofu hawa walibatizwa kwa maji mengi na siku ya Jumatatu na Jumanne walianza masomo yao ya kukulia wokovu katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" jijini Dar es Salaam.

Kama unahitaji kumpokea Yesu Kristo kuwa BWANA na mwokozi wa maisha yako, tunakualika katika ibada ya Jumapili hii hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Kanisa limeandaa usafiri wa bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho na Mwenge kwenye mataa jijini dar es Salaam.

Mch. Elizabeth Lucas
































Mch. Francis Machichi




















Comments