RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

14.01.2018: AMSHUKURU MUNGU KWA MAPITO ALIYOPITIA

Tunaambiwa tumshukuru Mungu kwa kila jambo. Tumshukuru Mungu wakati wa shida na raha. Mungu ni mwema na ni mwaminifu kwa kila mtu. Unapopatwa na gumu endelea kumshukuru Mungu na kumuomba akuepushe na hilo jaribu. Unapobarikiwa endelea kumshukuru Mungu ili azidi kukubariki.

Hivi ndivyo huyu muumini alivyomshukuru Mungu kwa yale yaliyomkuta. Hii ilikuwa ni siku ya Jumapili 14.01.2018 katika ibada ya KUSHIKWA MKONO NA MUNGU iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Yawezekana unapitia gumu lakini umemsahau Mungu, imefika kipindi unasema Mungu hayupo. Nakusihi, wewe endelea kumuangalia huyu Mungu wakatika wa shida na raha, Kila jambo linamakusudi katika maisha yetu ya hapa duniani. Usimwaache Mungu hata kidogo.
Washirikishe watumishi wa Mungu nao watakupa muongozo sahihi katika hilo jaribu lako. Na siku ya Jumapili tutakuwa na ibada hapa Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare amejipanga kukuhudumia akishirikiana na makuhani 12





Comments