RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MUSIC VIDEO | MUSIC AUDIO: BOMBY JOHNSON – HAKUNA JAMBO




Mwimbaji mahiri wa nyimbo za Injili Tanzania Bomby Johnson amefanikiwa kutimiza azma yake ya kufanya video yake ya kwanza toka aanze huduma yake uimbaji ambapo leo kupitia channel yake ya Youtube ameachia video yake iitwayo ”Hakuna Jambo”, ikiwa imeongozwa na director Einxer kutoka studio za Maxum Vision.

Hakuna Jambo ni wimbo unaokupa habari njema na matumaini ndani ya Moyo wako na kukupa nafasi ya kumtafakari Mungu kwa kiwango cha pekee na kukurudisha kwenye nafasi ya kuanza tena kwa upya ukiwa na nguvu inayomtegemea Yesu Kristo kwa maana kwake hakuna jambo linaloshindakana.

Bomby Johnson ambaye licha ya kuwa mwimbaji wa muda mrefu hakuwahi kufanya video yoyote kati ya nyimbo zake ambazo tayari ameshaziachi anakiri kuwa huu ndio wakati wa Bwana aliokuwa anausubiri kwa shauku kubwa na hakika amemuoa Mungu katika kiwango cha juu sana kwakuwa sasa amepata menejimenti mpya iitwayo Brand Exponentials ikiwa ni kampuni pekee aliyoingia nayo mkataba katika kusimamia kazi zake za muziki ndani na nje ya Tanzania na ameahidi kuwa ataendelea kufanya kazi bora zaidi katika kiwango cha kimataifa kwakuwa yeye ni mwanamuziki wa kimataifa.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii ya pekee na upakue wimbo huu uliobeba habari njema kwako ili ubarikiwe na uinuliwe. karibu!!

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Bomby Johnson kupitia
Simu/WhatsApp: +255 712 496 727
Facebook: Bomby Johnson
Instagram: @bombyjohnson
Email: bombyjohnson@gmail.com
Website: www.bombyjohnson.com

Comments