RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

MUSIC VIDEO | AUDIO MUSIC: EDDAH MWAMPAGAMA FEAT WALTER CHILAMBO – UNAJUAGA

Mbali ya kuwa ni video nzuri sana na yenye kubariki, ”Unajuaga” pia ni wimbo uliojaa unyenyekevu kwa Mungu ukielezea vile mtu anaweza kurudi katika Imani ya kumtegemea Mungu kuliko kitu kingine kwakuwa yeye ndiye anayefahamu undani wetu na uhalali wa maisha yetu, Kama Mungu alituumba kwa mfano wake basi yatupasa sisi kama watoto wake kumsifu na kumtumika Yesu Kristo katika roho na kweli ili atushindie katika kila vita tunayopigana kiroho na kimwili kwakuwa anatujua vyema..

Hakika hii ni moja kati ya video nzuri sana na wimbo wenye kubariki mno katika mwaka 2017 na hakika utakuwa shuhuda wa nuru mpya ya matumaini ndani ya moyo wako na kumtafakari Mungu kwa namna ya pekee sana.

Kwa moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video video na kupakua wimbo huu ambao ni hakika utakubariki na kukuinua sana!

Comments