RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

BERTHA KAPUFI – MAOMBI





Kutoka mjini kibaha maili moja leo kwa utukufu wa Mungu namleta kwako mwimbaji wa nyimbo za Injili anayefahamika kwa jina la Bertha Kapufi ambaye baada ya kimya cha Muda mrefu sasa amekuja na ujio wake mpya wa video iitwayo Maombi, video hii imeongozwa na director anayefahamika kwa jina la Yona Mkumbwa kutoka studio za YTM IMAGE na wimbo ukiwa umetayaarishwa ndani ya studio Non Stop Records chini ya mikono ya prodyuza GS.

”Maombi pekee ndio jibu kwa shida yoyote, vikwazo, majaribu na matatizo mbalimabali katika maisha ya binadamu, hivyo mara tupatapo matatizo tumweleze Mungu kupitia Maombi naye atatenda maana amesema niite nami nitakuitika………kupitia Maombi majibu ya matatizo yetu yanapatikana.” – Bertha Kapufi

Hakika hii ni video nzuri iliyojaa ujumbe wa kiroho unaotukumbusha umuhimu wa Maombi katika kuhuisha na kuboresha mawasiliano yetu na Mungu.

Kwa Moyo mkunjufu nakukaribisha kutazama video hii na kupakuwa wimbo huu ambao ni hakika utakubarikiwa sana.. Karibu!!

Kwa mawasiliano zaidi na mialiko ya huduma wasiliana na mwimbaji Bertha Kapufi kupitia:
Simu/WhatsApp: +255 712 676 337
Facebook: Bertha Kapufi
Instagram: @berthakapufi
Youtube: Eddah Solomon

Comments