RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

29.10.2017: MAELFU YA WATU WAINGIA KWENYE KISIMA CHA BETSAIDA KATIKA IBADA YA KUTENGUA MANUIZO NA LAANA.

Maelfu ya watu waingia kwenye kisima cha BETSAIDA katika ibada ya maombi ya KUTENGUA MANUIZO NA LAANA KATIKA MAISHA YETU. Hii ilifanyika siku ya Jumapili 29.10.2017 katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" baada ya ibada na maombezi kumalizika. Maelfu ya watu waliacha shida zao, mikosi, majini, mapepo, magonjwa, ugumba, upofu, nguvu za giza, kukosa kibali na promosheni, tabia ya kutopenda mambo ya Mungu, hali ya kutaka kujiua kutokana na changamoto za kimaisha , waliacha kila kitu kibaya kinachotokea maisha yao ndani ya Kisima cha Betsaida kilichhombewa na Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.

Baadhi ya watu walichota yale maji kwa IMANI ili wakayatumie majumbani mwao au kwa wagonjwa walioshindwa kufika kanisani kutokana na magonjwa yao. Wakati wa kudumbukia/kupita katika Kisima cha Betsaida baadhi yao walianza kulipuka mapepo, majini huku wakitokwa na nguvu za giza, kwasababu ndani ya kile kisima kulikuwa na Nguvu za Mungu.

Tendo hili la kuingia kwenye Kisima cha Betsaida huongozana na tendo la IMANI. Watu wanapoingia katika maji haya yaliyoombewa na watumishi wa Mungu HUAMINI kuwa Yesu mtenda miujiza ataondoa kila kitu kibaya katika maisha ya watu.

Katika zoezi la kuingia katika kisima hiki, Mhe. Bishop Rwakatare alikuwa ni mtu wa kwanza kuingia kwenye kisima hicho akifuatiwa wa wazee wa kanisa na wachungaji. Na kupitia Kisima hiki wapo watu wengi waliopoma magonjwa, waliofunguliwa na nguvu za giza, waliooa na kuolewa, waliopata kazi, waliopata safari za Ulaya, waliopata kibali katika kazi zao, waliolipiwa madeni, waliopata kodi za nyumba, walioinuliwa n.k

Tunakukaribisha katika ibada ya Jumapili hii kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana hapa Mlima wa Moto Mikocheni “B”. Kutakuwa na usafiri bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada kumalizika utarudishwa kituoni.

Mh. Bishop Dr. Gertrude akiwa wa kwanza kuingia kwenye Kisima cha betsaida


































Comments