RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

17.09.2017: VIONGOZI WA CHAMA CHA WANAWAKE/WAMAMA (WOCA) WALIVYOHIMIZA WATU KUTOKOSA KONAMANO LA MWANAMKE NA UCHUMI - MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Katika ibada ya MAOMBI YA KUFUFUA VITU VYETU VILIVYOKUFA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 17.09.2017 Chama Cha Wanawake au Wamama (WOCA) wa Mlima wa Moto Mikocheni "B" waliwahimiza watu kuhudhuria KONGAMANO LA WANAWAKE NA UCHUMI LA KUKOMESHA KILIO CHA MWANAMKE Kiuchumi, Kiafya na Kifamilia. Katika kongamano hilo kutakuwa na masomo kama vile:-
1. Mwanamke na Uchumi.
2. Nafasi ya Mwanamke katika nyumba/Kanisa.
3. Mwanamke na Huduma na
4. Usimamizi wa familia (mume na watoto)

Kongamano hili ni la siku 8 na litaanza rasmi Jumapili hii 24.09.2017 hadi Jumapili 01.10.2017 ndani ya kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" kuanzia saa 9 alasiri hadi saa 1 jioni kila siku. Siku za Jumapili litaanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana.

Wahubiri na walimu watakaofundishi na masomo ya Mwanamke na Uchumi ni
1. Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare.
2. General Apostle Dr. Dunstan Maboya
3. Dr. Peter Mitimingi
4. Esther Mukasa
5. Chriss Mauki.

Waimbaji watakaoimba siku hiyo ni:-
1. Bahati Bukuku.
2. Daughter of Zion.
3. Kikonko.

Kuna vitambaa vya sale vimeandaliwa kwaajili yako na vinapatikana katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B". Ukifika hapo uliza ofisi za utawala watakusaidia.

Wewe ambaye ungetamani kuchangia Konamano hili kwaajili ya kazi ya BWANA, kadi zinapatikana kanisani Mlima wa Moto Mikocheni "B".

Konamano hili limeandaliwa kwa wanawake wote kutoka makanisa mbalimbali, dini mbalimbali, mataifa mbalimbali, makabila yote na hakuna kiingilio.

Siku ya Jumapili tu, usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye Mataa, barabara ya Coca Cola. Baada ya ibada utarudishwa kituoni.


Janeth Urasa (kushoto) akiwahimiza watu kutokosa kongamano la Mwanamke na Uchumi







































Comments