RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

17.09.2017: MAOMBI YA KUBARIKI KAZI YA MIKONO YETU YALIVYOFANYIKA KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

Katika ibada ya MAOMBI YA KUFUFUA VITU VYETU VILIVYOKUFA iliyofanyika katika kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni "B" siku ya Jumapili 17.09.2017 Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare aliongoza maombi ya MAFANIKIO KATIKA KAZI YA MIKONO YETU. Na hivi ndivyo alivyoongoza maombi. 

Tusome Kumbukumbu la Toarati 28:12, “Kila utakachokishika katika mkono wako, Mungu atakibariki”. Na kuanzia sasa kila utakashika au kila mradi utakaouanzisha, kila kazi utakayofanya kwa mikono yako itabaraikiwa kwa jina la YESU. Sasa nyoosha mikono yako mbele kama unapokea kitu na sema, “Ewe mikono yangu, wewe umebarikiwa, neno la Mungu linasema, “Kila kitu nitakachokishika kwa mikono yangu, Mungu utakibariki”, Ewe mikono yangu, mbona sioni Baraka? Sasa naichovya mikono yangu kwenye damu ya Yesu, kama nimelogwa nisitajiriki, leo uchawi umeshindwa kwa jina la Yesu, Kama nimefungwa na wachawi, kwa damu ya Yesu ninajifungua katika jina la Yesu. Ewe mikono yangu, kuanzia sasa utashika pesa nazo zitakaa. Wewe jinni chuma ulete, huna mamlaka na pesa zangu kwa jina la Yesu. Kuanzia sasa sitafanya kazi bila faida, Mungu atanibariki kwa jina la Yesu. Ninakabisdhi biashara na kazi zangu za mikono yangu mikononi mwako Mungu kwa jina la Yesu. Kuanzia sasa umaskini bye bye, mikono yangu itahesabu pesa, malaki, mamilioni, nitapokea ma-Dollar, ma-Paund, ma-Euro kwa jina la Yesu. Sasa naomba uombe mwenyewe kwa kuitamkia mema mikono yako.
Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare

Mch. Antony Mwakibete












































































Comments