RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

03.09.2017: LAMECK KIBUGU AFANYIKA BARAKA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI "B"

"ZABURI 103:1. Ee nafsi yangu, umuhimidi BWANA, naam vyote vilivyo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. 3. Akusamehe maovu yako yote, akuponya magonjwa yako yote; akukomboa na uhai wako na kaburi"
upa pumzi nyingi yakupasa kumhimidi BWANA kwani wapo wengi sana walitamani kupata pumzi kama yako lakini walishindwa. 
Unapopata nafasi kidogo jitahidi kumsifu Mungu kwa nyimbo na kucheza huku ukimuomba Mungu akusamehe maovu yako yote. Mungu akikusamehe maovu yako anasema anauwezo wa kukuponya na magonjwa yako yote. Kwahiyo ukihitaji uponyaji ni vyema ukassamehe na kutenda yaliyo mema mbele za Mungu
Siku ya Jumapili 03.09.2017 tulibarikiwa sana na wimbo kutoka kwa mwimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Kenye. Wakati akiimba tuliona uwepo wa Mungu katika ibada hii ya KUPOKEA HABARI NJEMA. Tuna kila sababu ya kumshukuru Mungu pamoja na mwimbaji Lameck Kibugu kwa kujitoa kutoka Kenya kuja Mlima wa Moto Mikocheni "B" kwa kazi ya Mungu. Tunamuombea Mungu aibariki huduma yake na ampe ufunuo wa kutunga nyimbo zenye kutubariki na kumuinua Kristo.

Kwa wale waliokosa kufika katika ibada iliyopita, sasa tunakualika rasmi katika ibada ya Jumapili itakayoanza saa 3 asubuhi hadi saa 8 mchana. Usafiri ni bure kuanzia kituo cha mabasi cha Makumbusho au Mwenge kwenye mataa barabara ya Coca Cola
Lameck Kibugu











  








Comments