RUMAFRICA Magazine

RUMAFRICA FASHION

RUMAFRICA FASHION

Gama Mwasumbi: MWANANUME USITUPE LAWAMA KWA MWANAMKE




Kuna kitu ambacho kwa Ufunuo wangu (Mimi Gama) nafikiri Adamu kama angekifanya mapema pale bustanini kingemsaidia sana Eva kutorubuniwa kirahisi na Shetani.

Wanaume wengi sana hutupa lawama kwa Wanawake pale wanapokosea bila kujua kwamba ni sawa sawa na kujipigisha kelele mwenyewe.

Adamu alipoumbwa na kukabidhiwa ile bustani ya Eden,Mungu alimpa kila kitu akitunze na alimpa maelekezo yote kuhusu ile bustani pamoja na kile kilichokatazwa na Mungu kisiguswe.


Wanaume wengi sana dunia hii Mambo yao mengi hayaendi sawa kwasababu ya kutokumuhusiisha Msaidizi mambo yao muhimu maishani.
Kuna watu leo wamekufa na wakaacha familia zao zikiteseka kwasababu ya usiri wa vitu vya maendeleo wanavyovifanya.

Kusudi la Mungu kumleta Eva ilikuwa ni kumsaidia Adamu afanye kazi aliyokabidhiwa na Mungu kwa urahisi zaidi.(MSAIDIZI)
Sidhani kama Adamu alimpa details zote mke wake kiundani kama ilivyotakiwa.

Kwa taarifa yako hakuna mtu mlinzi wa Mali zako kama mkeo.
Kwanza kitu cha kwanza huwa akilini mwake ni Familia yake.
Mwanamke ana uwezo wa kuvumilia Machungu kuliko mwanaume.
Na ukimpa maagizo yoyote ya faida na mkakubaliana,huwa hawezi kwenda kinyume na hayo hata aje nani.

MEN

MUNGU anapokuletea Mwanamke (Mke) Maishani mwako,kuna vitu ambavyo amempa vinaweza kukusaidia kuwa Mwanaume bora ambaye Mungu angetaka uwe.(Anakukamilisha)
Unapokuwa humpi uthamani wake kwako kuna uwezekano mkubwa sana wa kutokuifikia hatima ambayo Mungu alitaka uwe.

Mpende,Muheshimu,Msikilize,unaweza ukagundua Madini adimu sana Mungu aliyoweka ndani ya hawa viumbe.

Usiwe mbishimbishi tu unayepuuzia Mawazo yake kila anapojaribu kukushauri kitu.
Mpe nafasi ya kusikilizwa na pia usipende kuchukua mawazo kwa rafiki zako kila wakati,wakati huyu ndiye mtu ambaye Mungu amekupa mjenge familia pamoja.

Marafiki comes and go lakini mkeo ndiye atakaekuwa nawe kwa shida na raha.Ndiye atakayelia nawe na kucheka nawe.
Ukitaka kufanikiwa na Mungu abariki Uchumi wenu,Basi jifunze kutokumficha mkeo chochote.

Comments