Select Menu

News

TAMASHA LA MAOMBI

TAMASHA LA MAOMBI

UBUNGE

UBUNGE

MCH. BURTON SANGA

MCH. BURTON SANGA

JIFUNZE KIFARANSA

JIFUNZE KIFARANSA

TTCL

TTCL

GEPF

GEPF

VIGAE TANGAZO

VIGAE TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

IRINGA MAZIWA TANGAZO

AZAM TV

AZAM TV

RUMAFRICA NA HABARI ZA GOSPEL: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA Online MAGAZINE: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

Rumafrica. Powered by Blogger.

RUMAFRICA Online TV: Bonyeza alama nyekundu kusoma zaidi

RUMAFRICA: MATANGAZO: Bonyeza alama nyekundu

ELIMIKA NA RUMAFRICA

RUMAFRICA MTAANI

MLIMA WA MOTO ONLINE TV NA HABARI MBALIMBALI ZA MLIMA WA MOTO

RUMAFRICA VIDEO

Siku ya Jumapili 23.04.2017 ya KIPOKEA HABARI NJEMA katika  kanisa la Mlima wa Mlima wa Moto Mikcheni “B”, Mh. Bishop Dr. Gertrude Rwakatare alisisitiza kanisa kuwa na umoja na kuwa na lugha moja, na hivi ndivyo alivyoanza kusema;
Bwana asifiwe sana. Tusome Neno la Mungu kitabu cha Mwanzo 11:1-9, Biblia inasema, “ Nchi yote ilikuwa na lugha moja na usemi mmoja ikawa watu waliposafiri, pande za mashariki waliona nchi tambarare katika nchi ya Shinari wakakaa huko. Wakaambiana, haya na tufanye matofari tukayachome moto. Walikuwa na matofali badala yam awe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, haya na tujijengee mji na mnara na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina, ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akashuka ili auoni mji na mnara, waliokuwa wakiujenga wanadamu. Bwana akasema Tazama watu hawa ni taifa moja na lugha yao ni moja na haya ndiyo wanayoanza kufanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. Haya na tushuke  huko tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. Basi Bwana akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote, wakaacha kuujenga ule mji. Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli, maana hapo ndipo Bwana alipoichafua lugha ya dunia yote, na kutoka huko Bwana akawatawanya, waende usoni pa nchi yote.”

Nitasema kwa ufupi, lakini lengo la ujumbe huu ni tuombe kwa ajili ya kanisa letu. “Ninaomba kwa ajili ya umoja wa kanisa, ninaomba kwa ajili ya mshikamano wa kanisa letu.”  Nilipokuwa safari (afrika Kusini) Mungu alisema na mimi utakaporudi  nyumbani, chukua muda mwingi hata kama ni mwezi mzima kuligusa kanisa, kugusa mioyo ya kila mmoja waweze kurudi katika upendo ule wa kwanza tulioanza nao.

Ndugu zangu tulipewa amri mpya katika Yohana 13:34 Yesu kasema,  “amri mpya nawapa pendaneni”, anasema pendaneni mpaka wamataifa wajue kweli ninyi ni wanafunzi wangu. Na kweli ukiingia katika kanisa la watu wa Mungu kitu cha kwanza kitakachokugusa ni upendo wao kwa sababu hata kama hakujui atakuuliza, na mimi nilitokea katika dini ya Romani Katoliki ambako watu wanaposalimiana wanakumbatiana kama ishara ya upendo. Nilipokuwa Katoliki baadae nikaanza kuelewa kuwa ule ulikuwa ni upendo wa kweli, waliwatambua wapendwa Wakristo kwa sababu ya kupendana kwao.

Upendo ule wa kwanza urudi tena nyumbani mwa BWANA, tukitoka nje tusisalimiane tu tunaojuana, tusalimiane na wageni, wakina mama, wamama, wengine wanakuja kanisani lakini hawana upendo wa kweli. Kama wewe unakaa kule shuka nenda kamtafute mama mwingine awe rafiki yako, tusikae wenyewe kwa wenyewe tu, kanisa litaongezeka kama kila mtu atachukua rafiki nyumbani mwa Bwana. Umoja unamtisha hata Mungu, na umoja ndio ulioweza kusimamisha falme za Kiarabu, falme za Kiarabu ziliweza kusimama kwa sababu walikuwa na umoja hawakuweza kumtoa Sadam Husseni kwa sababu walikuwa na umoja, walikuwa na mshikamano, walimpenda, hawakuweza kumtoa Gadafi kwa sababu walikuwa na mshikamano, lakini mitandao ilivyokuja, na utandawazi ulivyokuja vijana wakaanza kutuma message kuwa hawa wazee yaani Sadam na Gadafi tuwatoe madarakani  na ndio ukaona falme za Uarabuni zikaanza kusambaratika.

 Umoja unafanya tusimame pamoja, na Yesu kabla ya kuondoka kitabu cha Mathayo 17 kinasema,  akasema, “Nimewaombea hawa wachache ambao wao wamemwamini Kristo, wawe na umoja kama sisi tulivyo na umoja, umoja ni nguvu ya kanisa, hapa tunaona wenzetu katika kitabu cha Mwanzo 11, walikuwa wameshikamana wakiwa na lugha moja nia moja ya kujenga mnara mmoja ili wakamuone Mungu, wakaanza kujenga, Mungu alivyochungulia akaona mnara karibu unatoboa, akasema hawa watu tusipoenda kutawanya mbinu zao, hakika wataingia hapo. Na ndio leo hii unaona kuna lugha tofauti kama vile Kinyakyusa na lugha mbalimbali ziliingia.  Anasema wakashindwa kusikilizana, kiongozi akisema,  leta tofali huyu analeta panga yaani analeta kitu tohfauti kwasababu hawasikilizani kutokana na lugha kusambaratishwa, kuanzia hapo  kujenga mnara kukaisha hapo wakaamua wakabomoa mnara wao.

Katika kila ushirika kama hakuna lugha moja, nia moja hamuwezi kufaulu, lakini mkishikamana mtafanya makubwa. Sisi ni familia ya Kristo, sisi ni watu wa Mungu ni mfano kwa wamataifa, tukishikamana tutafanya makubwa, tukishikamana watajua kuwa tumeokoka, tukishikamana Dar es Salaam itaokoka, tukishikamana kanisa hili tutalivunja tutajenga kanisa la ghorofa, bila kujari unapesa au hauna pesa, tukishikamana watu wengi wataongezeka kanisani kwa sababu wataona tumeokoka, watu wengi wanaangaliaga hawa watu wapoje, wakiona tun watu hawaelewani wahawezi kuja kanisani lakini wakiona watu tumeshikamana, tuna umoja, tunatembelea kama hivi tunatembeleana, hapo ndipo unakuta mtu anasema hii familiya nzuri acha nijiunge nayo kwahiyo ningependa kukuasa hata kwa viongozi, sisi ndio barua iliyowazi kwa wengine, lazima sisi kwa sisi tushikamane, lazima sisi wenyewe tupendane, mmeacha historia, mmeacha mtetemeko Dodoma, mmeacha simulizi Dodoma kwa ajili ya umoja wa kanisa hili viongozi mbalimbali wanakuja walikuja ili kuungana nasi katika sherehe hii ya furaha   ya kuapishwa kwangu huu ni umoja wetu wa kanisa, wanasema jamani hawa watu ni wa namna gani, wale waliovaa sale nyekundu wakapiga picha, watu wakasema mama yangu ni nini hiki sijawahi ona, wakina baba wameva suti zao nyeusi ta tai nyekundu watu wakashangaa kwa sababu ya umoja nawasihi ndugu zangu mbalimbali, karibuni Mlima wa Moto, kanisa ni safina, ndani ya safina kuliingia nyoka, ndege, samba, mbwa, kuliingia wanyama wa kila aina wawili kwa wawili, lakini midomo ilifungwa ya samba asione mbuzi, midomo ilifungwa asiweze kummeza mbwa, unajua kiasilia mbwa na chatu, kama kuna kumaku, chatu akiachama mdomo mbwa analia mwenyewe anajipelea anajua anaenda kumezwa sasa sumaku inamvuta, lakini midomo ya chatu ilifungwa kwa sababu ilikuwa kwa ajili ya umoja na hapa kanisani kwetu sisi tuwefamiliya moja lazima tuwe wamoja aliyejuu ashuke ammbebe wa chini tukisaidiana kanisa tutasonga mbele, tukibebana kanisa litaendelea tuko hapa kwa ajili ya kusaidiana, tuko hapa kwa ajili ya kuujenga mwili wa Kristo, huwezi kumuona Mungu mzimamzima lakini mimi nitakapo kusaidia ndio Mungu ananitumia kwa mfano wake tu, kwa hivyo lazima tujishuhulishe katika misingi ya kupendana, kushikamana, kuchukuliana tofauti zetu tuziache, sisi ni ndugu, sisi ni wamoja, mimi nikipata na yeye kapata ndio maana tunachukua simu zenu, mkiwa na shida msikwame tukusaidie ili tukubebe, tukukwamue, mimi ni mama yenu wa kiroho na mama lazima nijari maisha yako. Mungu anajari umoja, na Mumngu anajali tunapochukuliana na Mungu anaribariki kanisa ukisoma Matendo 2:41 Nao waliolipokea neno lake wakabatizw, na siku ile wakaongezeka watu wapata elfu tatu. Wakawa wakidumu katika fundishola mitume na katika ushirika na katika kuumega mkate na katika kusali. Kila mtu akaingiwa na hofu, ajabu nyingi na ishara zikafanywa na mitume. Na wote walioamini walikuwa mahali pamoja na kuwa na vitu vyote shirika, wakauza mali zao na vitu vyao walivyokuwa navyo na kuwagawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. Na siku zote kwa moyo mmoja, walidumu ndani ya hekalu, wakimega mkate nyumba kwa nyumba na kushiriki chakula chao kwa furaha na kwa moyo mweupe. Wakimsifu Mungu na kuwapendeza watu wote. Bwana akalizidisha kanisa kila siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa. Umoja ukaleta maajabu nyumbani mwa Bwana, Mungu anashuka na anaonekana.        


Mh. Bishop Dr. Gertrude RwakatareNapenda chapati haswa aliyoipika mama. Nikila na maharage huwa nashiba zaidi. Sijui kama na wewe unapenda chapati.

Leo Nataka tujifunze kitu kutoka kwenye chapati. kabla ya kuwa chapati ilikuwa ngano. Ngano ambayo ukiitazama haivutii inafanana na unga wa mahindi au chokaa laini. Ngano ambayo inaweza kutoa vitafunwa vya namna mbalimbali kama vile maandazi,vitumbua, keki, mikate n.k. Hivyo karibia kila mtu mwanzo huwa kama ngano kabla ya hajaamua awe chapati,mkate,maandazi au keki.

Chapati kabla ya kuwa cha chapati ilikuwa ngano. Ilipoanza kuwa chapati ilikandwa, ilichanganywa na maji ya moto au baridi na mafuta kidogo na mkaandaji anaanza kukunda. Anatumia nguvu nyingi kukanda. Ndivyo ilivyo ukiamua kuwa mtu Fulani lazima ukubali kukandwa, ukubali kuchanganywa na maji ya moto ili ukandike vizuri. Dunia inaweza kukuchanganya na kujiona huvutii au hufai,kumbuka na chapati pia hupitia sura hiyo ya kutokuvutia.

Mara umejifunza hili matokeo yake unafeli wala usikate tama jua ndo kukandwa huko ili uweze kufikia malengo yako.

Ngano inapomalizizwa kukandwa huwekwa kwenye kibao cha kusukumia. Huanza kusukumwa na kuchongwa kuwa kwenye umbo la chapati. Unaweza ukawa unajiona ueshakuwa mwanamziki kumbe bado ndio kwanza unasukumwa kuwa mwanamziki. au kazi ,mfanyabiashara au kazi yeyote ile. Inakubidi utulie na kukubali kutengenezwa. Wala usiwe na haraka kuwa na umbo la chapati hukumaniishi ushakuwa chapati.

Ikishatoka kwa kibao na kuwa na umbo la chapati.Hupelekwa jikoni.huwekwa juu ya kikaango bila kupitia katika changamoto. huwezi kuwa vizuri katika fani au taaluma unayotaka kuwa bila kupitia changamoto tambua ya kuwa changamoto ni sehemu ya mafanikio yako.

Kama vile ambavyo dhahabu ili ing’ae vizuri hupitishwa katika moto ndivyo na wewe ili uwe mwenye manufaa katika jamiilazima upitie changamoto. Chapati isipopitia katika moto wala huwezi kuila maana tumbo laweza uma.Ndivyo hata wewe usipopitia changamoto mafanikio hayawezi kuja.

Ndivyo ulivyo kwa kila mtu unayemuona ni maarufu au aliyetenda makubwa katika sayari hii.Kabla hajawa hivyo alikuwa mtu wa kawaida sababu kabla haijawa chapati ilikuwa ngano. Sasa sio wote tutakuwa chapati, Wengine watakuwa maandazi lakini nayo kuna hatua yamepitia ambayo sio lakini tofauti sana na chapati.

changamoto za kimafanikio hutofautiabna kama ilivo chapati huiwekwi amira maandazi huwekwa amira.Tambua mafanikio bila changamoto hayakamilika.lazima upitie kama yalivo maamdalizi ya chapati. Pia usikate tama kwa kile kinachotokea katika maisha yako bali pambana.
Karanga ni mojawapo ya mazao yanayotoa mafuta. Katika Tanzania zao hili hustawi zaid katika mikoa ya Kusini Mashariki, Dodoma na Morogoro,Mikoa ya Kanda ya ziwa Shinyanga na Geita, pia Kilimanjaro, Mbeya na Mikoa mingine ya Tanzania. Pamoja na kutoa mafuta vile vile zao hutumika kwa njia nyingine mbali mbali,

Nazo ni pamoja na: 

1. Chakula cha wanyama (Mashudu na majani)
2. Kurutubisha ardhi
3. Chakula cha binadamu (Confectionary)

Kwa ujumla zao hili hutumika na wakulima kama zao la biashara.

HALI YA HEWA
Karanga hustawi vizuri katika maeneo yaliyopo kwenye miinuko chini ya mita 1500, toka usawa wa bahari katika Tanzania, na hustawi zaidi katika maeneo ambayo yanapata mvua za wastani wa mm 750 hadi mm 1200 kwa mwaka.
Vile vile karanga hustawi vizuri kwenye udongo wa kichanga, inashauriwa kutopanda karanga kwenye udongo mzito (mfinyanzi) hii ni kutokana na sababu kwamba, karanga hazistawi kwenye sehemu zinazo simama maji, na udongo mzito huleta hasara wakati wa uvunaji.

AINA ZA KARANGA
Kuna aina kuu tano bora za karanga ambazo zimetolewa kwa wakulima hapa nchini.

a. Red Mwitunde 
Ilitolewa kwa wakulima miaka ya 1950.
Mbegu za muda mrefu (Virginia Spreading bunches).
Huchukua muda wa siku 120 -140 toka kupanda hadi kukomaa. Ina uwezo wa kutoa kilo1000 kwa hekta. Mbegu zake ni kubwa na zina rangi nyekundu.

b. Nyota
Ilitolewa mwaka 1983.
Mbegu ya muda mfupi ( Spanish Errect Banch).
Huchukua siku 90-100 tangu kupanda hadi kukomaa. Ina uwezo wa kuzaa wastani wa kilo1500 kwa hekta. Mbegu zake ni ndogo, na zina rangi ya udongo (Tan).
Aina hii ya mbegu zina tabia ya kuanza kuota tena shambani mara tu zikiisha komaa, hivyo ni muhimu kuzivuna mapema zikisha komaa.

c. Johari:
Ilitolewa mwaka 1985.
Mbegu ya muda wa kati (Virginia Spreading Bunches).
Huchukua siku 110 - 120 toka kupanga kuvuna. Mbegu zake ni kubwa na zina rangi ya udongo (Tan). Ina uwezo wa kutoa wastani wa kilo 1000 kwa hekta moja.

d. Pendo: . 
Ilitolewa mwaka 1998.
Mbegu ya muda mfupi ( Spanish Errect Banch). Huchukua siku 90-100 tangu kupanda hadi kukomaa. Ina uwezo wa kuzaa wastani wa kilo 1500 kwa hekta. Maganda yake ni laini na mbegu zake ni kubwa, na zina rangi ya udongo (Tan). Kama Nyota, aina hii ya mbegu ina tabia ya kuanza kuota tena shambani mara tu zikisha komaa, hivyo ni muhimu kuzivuna mapema zikisha komaa.

e. Sawia:
Ilitolewa mwaka 1998.
Mbegu ya muda wa kati (Virginia Spreading Bunches).
Huchukua siku 110 - 120 toka kupanga kuvuna. Mbegu zake ni kubwa na zina rangi ya udongo (Tan). Ina uwezo wa kutoa wastani wa kilo 1000 kwa hekta moja.

Pamoja na mbegu zilizotajwa, kuna aina nyingine nyingi za kienyeji (local varieties) zinazotumiwa na wakulima katika sehemu mbali mbali.

UTAYARISHAJI WA SHAMBA
Shamba litayarishwe vizuri kuwezesha udongo kupenyesha maji na mizizi kirahisi. Karanga hupandwa kwenye matuta au sensa (shamba tambarare).

UTAYARISHAJI WA MBEGU
Karanga ambazo zinakusudiwa kwa mbegu zitunzwe na maganda yake bila kubanguliwa. Zibanguliwe karibu na msimu wa kupanda na kuchaguliwa. Baada ya kuchaguliwa zitiwe dawa, aina ya Fernasan D, Katika uwiano wa gramu 28 za dawa kwa kila kilo 10 za mbegu safi.

WAKATI WA UPANDAJI
Uamuzi wa kuchagua wakati mzuri wa kupanda niule utakaoliwezesha zao hilo kukomaa wakati wa mvua za mwisho. Kuchelewa kupanda, hupunguza mavuno. Ni muhimu kuchagua aina ya mbegu ambazo uvunaji wake unafanana na mazingiza ya eneo hilo kihali ya hewa.

Kwa mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, karanga za muda wa kati na mrefu (Johari, Red Mwitunde) zipandwe kuanzia katikati, hadi mwishoni mwa mwezi Desemba. Karanga za muda mfupi (Spanish na Valencia) zipandwe kuanzia mwishoni mwa mwezi Desemba hadi katikati ya mwezi Januari.
Kwa mikoa ya Tanga, Morogoro na sehemu za mkoa wa Dodoma, karanga zipandwe mapema mwanzo wa mvua ndefu. (Februari/March).

NAFASI KATI YA MIMEA
Inashauriwa kupanda karanga katika mistari. Nafasi kati ya mistari ni sentimita 50, na kati ya mimea ni sentimita 15, kwa karanga zinazotambaa (Virginia Spreading types). Kama karanga zinapandwa kwenye matuta ya sentimita 90, zipandwe mistari miwili, kila tuta. Kwa nafasi hii kiasi cha kil 60-75 za mbegu hutumika kwa hekta moja.

Kwa karanga zilizopo kwenye kundi la Spanish/Valencia (zisizotambaa), nafasi kati ya mistari ni sentimita 50, na kati ya mimea ni sentimita 10. Endapo karanga zimepandwa kwenye matuta ya sentimita 90, panda mistari miwili , inayofanya nafasi sawa na sentimita50 kwa sentimita 10. Kiasi cha kilo 80-100 za mbegu hutumika kwa hekta moja kwa kutumia nafasi hii.Kwa ina zote za mbegu, panda mbegu moja safi, katika kila shimo.

MBOLEA
Kufuatana na majaribio yaliyofanyika imeonekana kuwa karanga hustawi vizuri chini ya viwango vidogo vya phosphorus (TSP, SSP). Vile vile katika sehemu nyingine, karanga zimefanya vizuri kwa kutumia samadi. Ubadilishaji wa mazao (Crop Rotation) husaidia kutunza rutuba, hivyo kupunguza kiasi cha mbolea kinachotumika.Karanga zinaweza kulimwa baada ya mahindi, ili kutumia masalia ya mbolea.

UPALILIAJI
Karanga zipaliliwe zikiwa changa. Shamba lililotayarishwa vizuri na kuondolewa magugu ya muda mrefu (Perrenial weeds) linaweza kupalliwa mara moja, kwa sababu karanga hukua haraka, na zinaweza kushindana na magugu. Baada ya kutoa maua, karanga zisipaliliwe, hii inaweza kuharibu 'pegs', hatimaye kupunguza mavuno.

MAGONJWA NA WADUDU WAHARIBIFU:
1. MAGONJWA

(i) Ugonjwa wa kuoza (Aflatoxin)
Katika hali ya unyevu mwingi vimelea viitwavyo Aspegilus flavus huota ndani ya maganda na kushambulia mbegu za karanga. Vimelea hivyo hutoa kemikali ambayo ni sumu.

KUZUIA


Hakikisha kuwa karanga haziharibiwi wakati wa kuchimba.
Hakikisha karanga zinakaushwa vizuri (Unyevu wa 10%) kabla ya kuzitunza zitumike kama mbegu
Karanga za kupanda zitiwe dawa aina ya Fernasan-D.

(ii) Ugonjwa wa Madoa na Kutu: (Cercospora Leaf Spots and Rust)
Magonjwa haya husababisha madoa ya rangi ya kikahawia hadi meusi kwenye majani.

Vimelea vinavyosababisha magonjwa haya viko vya aina tatu:


(a) Cersospora arachidicola. Husababisha Early Leaf Spot.
(b) Phaeoisariopsis personata. Husababisha Late Leaf spot.

Ugonjwa wa Early Leaf Spot hutangulia kuonekana, lakini magonjwa yote mawili yanaweza kujitokeza shambani kuanzia wiki 3-5 baada ya karanga kupandwa.

(c) Puccinia arachidis. Husababisha ugonjwa wa Kutu.

Kuzuia:


Kupanda mapema.
Kuondoa maotea ya karanga wakati wa kiangazi.
Tumia dawa aina ya Chlorothalonil (Daconil 2787)

Dawa huwekwa kiasi cha kilo l.6 katika lita 800 za maji kwa hekta moja, kila baada ya siku saba, kwa majuma machache kuanzaia maratu dalili za ugonjwa zinapoonekana.

Uchunguzi juu ya aina zinazostahimili magonjwa haya bado unaendele kufanywa kwenye kituo cha utafiti wa kilimo Naliendele.

(iii) Ugonjwa wa Rosette (Rosette virus disease)
Ugonjwa huu huambukizwa na wadudu waitwao "Mafuta" Aphids (Aphis craccivora). Mimea ambayo imeshambuliwa na ugonjwa huu hudumaa, na inakuwa na madoa ya njano.


Ugonjwa wa Rosette (Ukoma)
Kuzuia:


Kupanda mapema
Panda karanga zako shambani katika nafasi za karibu karibu.
Palilia na toa maotea shambani mwako.

(iv) Ugonjwa wa maganda matupu (Empty pods or pops)
Karanga zilizoshambaliwa na ugonjwa huu, huwa lazina mbegu (maganda matupu). Ugonjwa huu husababishwa na ukosefu wa madini ya Calcium (chokaa) kwenye udongo


Kuzuia:
Tumia Calcium katika hali ya Gypsum (Ca SO4) kwenye mimea au weka Chokaa (lime - CaO) kwenye udongo kabla ya kupanda. Ugonjwa huu uko kwenye mikoa ya kusini mwa Tanzania (Lindi, Mtwara na Ruvuma) na hushambulia sana karanga za muda mrefu kama vile Red Mwitunde.
Majaribio hapa Tanzaniia hayajathibitisha kuweka chokaa (Liming) kuwa ni jibu sahihi la kupambana na ugonjwa huu, lakini ili kupunguza, kupanda mapema ni muhimu.

2. WADUDU WAHARIBIFU
(i) Mafuta Aphids au "Mafuta" (Aphis cracivora)
Hushambulia karanga kila msimu, lakini athari yao kubwa ni kueneza ugonjwa wa Rosette. Wakati wa mvua nyingi huoshwa toka kwenye majani, hivyo hawaleti madhara.

Kuzuia:
• Kupanda mapema
• kupanda karanga karibu karibu

(ii) Groundnut hopper: Hilda patruelis
Hufyonza mizizi, "pegs", na karanga changa, hivyo husababisha majani kuwa manjano, kunyauka, na mmea kukauka ungali mchanga. Wadudu hawa hushambulia mazao mengine kama vile maharage, kunde. alizeti na korosho, hivyo kunahitajika mzunguko (rotation) mzuri wa mazao.

Kuzuia:
• Kwenye mashamba makubwa, inashauriwa kutumia dawa aina ya Aldrin au chloropyrifos, kuchanganya kwenye ardhi kabla ya kupanda.
• Kunyunyizia Dimethoate mara tu wadudu wanapoonekana.
• Kutochanganya na zao la korosho au mbaazi kwenye shamba moja na karanga.

(iii) Mchwa.
Kuna aina mbili za mchwa ambao hushambulia na kusababisha uharibifu kwenye zao la karanga.
Aina ya kwanza ni wale ambao hutoboa sehemu ya chini kwenye mzizi, au kutengeneza matundu, na hukaa kwenye mmea wa karanga wakati wote zikiwa shambani.
Aina ya pili ni wale ambao hukata matawi yanayokua au kutambaa. Uharibifu huu huonekana zaidi kwenye shamba jipya. Kuchelewa kuvuna kunaweza kusababisha kupotea kwa mazao mengi, kutokana na kuharibika kwa mizizi, na kusababisha karanga nyingi kubakia shambani wakati wa kuvuna.


Kuzuia:
Mchwa wanaweza kuzuiwa kwa kutumia dawa aina ya Alandrin 40% ya unga, kwa kiasi cha kilo 2.5 kwa hekta., Njia rahisi ni kuchanganya dawa na mbolea aina ya Phosphate(TSP au SSP) au mchanga na kumwaga shambani kabla ya kupanda karanga.

(iv) Panya:
Hushambulia sana karanga zinapoanza kuota, na wakati zinapokaribia kuvunwa.

Namna ya Kuzuia panya:
• Tumia dawa za kuua panya
• Mitego
• Kuwachimbua toka aridhini walikojificha.

(v) Ndege
Kama panya, ndege hasa kunguru hushambulia sana karanga kabla hazijaota (mara baada ya kupanda), zinapoanza kuota, zinapokaribia na wakati zimekwisha komaa.


Kuzuia
• Kutumia mitego
• Kuamia
• Kuweka (kutundika/kuning’iniza) mzoga au kunguru mzima shambani.

UBANGUAJI NA UTUNZAJI WA KARANGA
Kubangua karanga ni kazi ngumu. Mtu mmoja anaweza kubangua kiasi cha kilo 12-15 kwa siku. Karanga zilizopo kwenye kundi la Virginia hubangulika kirahisi, kuliko aina yaSpanish au Valencia. Mashine za kubangulia karanga hupatikana hapa nchini, zinarahisisha kazi, lakini tahadhari isipochukuliwa huharibu karanga.

Karanga zinazokusudiwa kutunzwa kwa muda mrefu, zitunzwe na maganda yake kwenye ghala. Ghala iwe kavu, yenye kupitisha hewa, na imara kuzuia wanyama waharibifu kama vile panya.Ubora na uwezo wa karanga kuota huanza kupotea mara baada ya kubanguliwa.
Kuna wakati unajikuta tumbo limechafuka kwa kujaa gesi, kuuma na hata kuunguruma, unahisi unahitaji kunywa dawa ili litulie. Katika makala ya leo utajifunza njia bora ya kutuliza mchafuko wa tumbo kwa kutumia vyakula badala ya dawa za kisasa ambazo hutuliza dalili na haziondoi tatizo.

Mara kadhaa chanzo cha ugonjwa gesi tumboni hutokana na vyakula na vinywaji vinavyochangia tumbo kujaa na ukosefu wa choo kwa muda mrefu huwa ni soda, ulevi (hasa bia), vyakula vyenye mafuta mengi na vyenye chumvi nyingi.

Vyakula hivyo vinapoingia tumboni, huwa na tabia ya kuchelewesha usagaji wa chakula na uondoaji wa uchafu kwenye utumbo, hivyo huwa kikwazo katika mfumo mzima wa usagaji chakula kwa urahisi.

vyakula vifuatavyo husaidia kuondoa gesi tumboni.

1. Papai.
Watafiti wamebaini kuwa tunda hili, lenye ladha tamu na harufu nzuri, huboresha mfumo wa usagaji chakula, husafisha utumbo, huzuia magonjwa ya uvimbe tumboni na huimarisha mfumo wa kinga ya mwili.

“Vitamini na virutubisho vya papai vina faida nyingi, lakini faida kubwa ya papai ipo kwenye kirutubisho (Enzyme) aina ya ‘Papain’ ambacho hujulikana kwa uwezo mkubwa ilionao wa usagaji mzuri wa chakula tumboni,”

2. Mtindi (YOGURT).
Hata kama wewe si mpenzi wa mtindi, jaribu kunywa na utaupenda, hasa uwezo wake wa kuondoa matatizo ya kujaa gesi tumboni pamoja na matatizo mengine. Mtindi mzuri ni ule ‘plain’ ambao haujachanganywa na ladha au vitu vingine kwa lengo la kuongeza ladha. Bakteria asilia waliyomo kwenye maziwa mtindi ndiyo hufanya usagaji wa chakula kuwa mwepesi.

Mwisho, ili kupata faida ya papai na mtindi kama ilivyoelezwa hapo juu, ni vizuri ukala mara kwa mara kama siyo kila siku, kabla au mara baada ya kula vyakula ambavyo vinaweza kukuletea shida tumboni, au ukaweka mazoea ya kula kila siku ili kuliweka tumbo lako katika hali salama.

Tunda aina ya tango hupatikana maeneo mengi duniani, watu wengi hupuuza kula tunda hili kwasababu ya kutokuwa na sukari yoyote katika tunda hili.

Ukweli utabaki kuwa pale pale kuwa tango husaidia vitu vingi mwilini kwa mfano hupunguza maumivu ya kichwa, viungo vya mwili, hupambana na ugonjwa wa Cancer, husafisha figo, kupunguza uzito, huweka sawa mfumo wa damu, hukupatia afya nzuri ya nywele na mengineyo.

Jitahidi kula matango kwa afya bora, kwani unaweza kukata kata kama kachumbali ukatia chumvi ili kuleta radha ya kula. Mimi binafsi hupenda kula matango ninapoyapatia nafasi, kwani hayana idadi maalumu ya kula, utakula kadri uwezavyo.
Rais Donald Trump kwa mara nyengine ameionya Korea Kaskazini

Rais wa Marekani Donald Trump ameaonya kwa mara nyengine kwamba mzozo mkubwa utaibuka na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa kinyuklia na ule wa kutengeza makombora.

Katika mahojiano na chombo cha habari cha Reuters amesema kuwa angependelea mzozo huo kukabiliwa kidiplomasia lakini amesema hiyo itakuwa vigumu kuafikia.

Bwana Trump alimpongeza mwenzake wa China Xi Jinping akisema amekuwa akijaribu kwa kila njia kuishinikiza Korea Kaskazini.

Awali waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani Rex Tillerson alisema China imeionya Pyongyang kutarajia vikwazo iwapo itafanya majaribio mengine ya kinyuklia.

Wakati huohuo Korea Kaskazini imetoa kanda ya video ya propaganda ikionyesha itakavyoishambulia Marekani.

Kanda hiyo inashirikisha ikulu ya Whitehouse na ndege ya kubeba ndege za kijeshi inayokabiliwa na inakamilika na ikulu hiyo ikilipuka.

KUNDI la majambazi 15 wakiwa na silaha za jadi na milipuko ya baruti limevamia kitongoji kisha kubaka wanawake, kujeruhi, na kupora fedha na madini usiku wa kuamkia jana.

Tukio hilo lililotokea katika Kitongoji cha Machinjioni kilichopo katika Kijiji cha Mugusu wilayani Geita na lilichukua takriban saa moja.
Majambazi hao walikuwa na nondo, mapanga, fimbo na milipuko ya baruti.

Katika tukio hilo, wanawake wawili walibakwa na watu tisa kujeruhiwa kwa silaha hizo, imeelezwa na kwamba watatu kati yao, akiwamo Mwenyekiti wa kitongoji, Abdul Hamza, walilazwa katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Geita.

Mbali na kubaka na kujeruhi, watu hao pia walipora kiasi cha fedha na gramu 30 za dhahabu, vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. milioni tano kisha kutokomea kusikojulikana.

Kufuatia tukio hilo, Jeshi la Polisi limepeleka makachero na askari wa kitengo maalum cha kupambana na unyanga’anyi wa kutumia silaha ili kuwasaka majambazi hao.

Jeshi hilo pia limewataka wahusika wa vitendo hivyo kujisalimisha kabla ya kukamatwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Lodson Mponjoli, aliyetembelea eneo la tukio, alisema kitendo hicho hakikubaliki na msako mkali umeanza.

Kamanda Mponjoli alisema kundi la majambazi hao lilivamia Kitongoji cha Machinjio saa sita usiku wa juzi na kuwaweka chini ya ulinzi kwa karibu saa moja baadhi ya wakazi wa eneo hilo.

Katika uvamizi huo, Kamanda Mponjoli alisema, watuhumiwa walivunja vibanda vya maduka na nyumba za makazi kisha kupora mali zikiwamo simu za mkononi, dhahabu na fedha taslimu vyote vikiwa na thamani ya zaidi ya Sh. milioni tano.

Kamanda Mponjoli alisema wakati wa kutekeleza uhalifu huo, watuhumiwa waliwajeruhi wananchi.

Imeelezwa kuwa ili kutekeleza azma yao, majambazi hao walilipua baruti zilizotengenezwa kienyeji kwa lengo la kuwatia hofu majirani waogope kufika kutoa msaada.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema watuhumiwa wa uhalifu huo ni vijana wenye umri wa miaka kati ya 20 na 30 na kwamba walitumia mapanga na fimbo kuwajeruhi.

Marco Mjema na mwenyekiti wa Kitongoji cha Mugusu, Emmanuel Mapalala, walisema katika tukio hilo, majambazi hao waliwabaka wanawake wawili.

Waliojeruhiwa katika tukio hilo pamoja na Hamza ni Damas Josiah na Sele Seif ambao wamelazwa pia katika Hospitali ya Rufani ya mkoa wa Geita.

Wengine ni Joram Abel, Ibrahim Daud, Sweetbert Nicholaus na Masinde Thomas ambao walitibiwa na kuruhusiwa kuondoka pamoja na wanawake wawili waliotendewa ukatili wa kijinsia (majina tunayahifadhi).
NI dhahiri sasa kuna hatari ya Chama cha Wananchi (CUF), kuingia vitani kwa kile kinachoelezwa kuibuka kwa vita ya madaraka na kuwania ofisi ya chama hicho.

Hatua hiyo inatokana na pande mbili zinazovutana kujiandaa kwa mapambano kutokana na kile kinachodaiwa kuwania ofisi kuu ya CUF iliyopo Buguruni, Dar es Salaam.

Wakati wabunge wa chama hicho wanaomuunga mkono Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad wakijiandaa kwenda kufanya usafi katika ofisi hizo Jumapili, wanachama wanaomuunga mkono Mwenyekiti wa chama hicho anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Profesa Ibrahim Lipumba, wamekuwa wakifanya mazoezi mazito kujihami dhidi yao.

Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dodoma, Mbunge wa Temeke, Abdalah Mtolea, alisema katika siku za karibuni ofisi yao imegeuka kuwa genge la wahuni, hivyo kuna uchafu mwingi.

“Aprili 30 mwaka huu siku ya Jumapili, wanachama ambao hatumuungi mkono Lipumba, tutakwenda katika ofisi zetu za Buguruni kwa sababu hivi sasa zimegeuka kuwa genge la wahuni, hivyo kuna uchafu mwingi, tutakwenda kusafisha.

“Tutafanya usafi huo ili ofisi yetu iendelee kuwa safi na wanachama wote watakaojitokeza waje na mifagio na madekio. Tutatoa kila uchafu ili viongozi halali waendelee kufanya kazi,” alisema Mtolea.

Alipoulizwa kwamba hawaoni kufanya hivyo kama kunaweza kuleta uvunjifu wa amani, alisema tukio lolote watakalokutana nalo watalisafisha.

“Sisi tunakwenda kusafisha ofisi yetu kwa sababu tangu Msajili wa Vyama amtambue Lipumba kuwa mwenyekiti, hatujawahi kwenda, hivyo hatuendi pale kwa ajili ya kuvunja amani, bali tunakwenda kusafisha chochote kisichostahili na hata Lipumba ni uchafu. Tunasafisha ili tufanye siasa,” alisema.

Kuhusu mgogoro wao kuwa mahakamani, Mtolea alisema kesi iliyoko mahakamani ni ya kupinga Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi kumtambua Lipumba.

“Jaji Mutungi au Mahakama hawajawahi kusema hata siku moja kuwa wanachama hatuna haki kufika pale ofisini, hivyo sisi tunakwenda kufanya usafi.

“Tumejiandaa kwa usafi, tukikutana na uchafu ambao hatukuutarajia tutausafisha,” alisema Mtolea.

Awali, Mbunge wa Malindi, Ally Saleh, aliunga mkono uamuzi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), kulaani tukio la baadhi ya waandishi wa habari kupigwa katika mkutano wa CUF.

Alisema bado hawajaona wajibu wa Serikali katika tukio hilo walilofanyiwa waandishi wa habari ambao walikuwa hawana hatia yoyote.

“Tunawapongeza na kuwaunga mkono TEF kwa kulishughulikia suala hili la waandishi wa habari kupigwa, lazima tuhakikishe kuwa waandishi wanafanya kazi kwa uhuru.

“Bado hatujaona wajibu wa Serikali katika hili wakilaani na kuwahakikishia waandishi wa habari kuwa wanafanya kazi zao kwa usalama,” alisema.

Wiki iliyopita, watu wasiofahamika waliovalia kininja wakiwa na bastola, walivamia mkutano wa wanachama wa CUF wanaomuunga mkono Maalim Seif na kuanza kuwapiga pamoja na waandishi wa habari waliokuwapo.

WAKARIBISHWA

Akizungumzia hali hiyo, Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya, alisema kuwa wao wamejiandaa kuwapokea wabunge hao na kueleza mikakati ya kundi hilo la wabunge kufadhiliwa na Chadema, ikiwamo kuhifadhi kundi la watu wanaodaiwa kuwa majambazi.

“Unajua hawa wa ajabu sana. Je, ni nani aliyewaambia ofisi hapa Buguruni ni chafu? Kama wanakuja wabunge wetu tunawakarisha sana kwa mikono miwili. Ila tunajua wanafadhiliwa na Chadema na kundi la majambazi wamelihifadhi eneo la Mbezi kwa Msuguri ili waje wafanye uhalifu hapa, nasi tunawasubiri,” alisema Kambaya.

CUF BUGURUNI

Wanachama wa CUF upande wa Profesa Lipumba, juzi hadi majira ya usiku walionekana wakiwa wanafanya mazoezi huku wakiimba nyimbo mbalimbali za hamasa.

MTANZANIA ilishuhudia watu hao wakiwa juu ya jengo la ofisi kuu za chama hicho zilizopo Buguruni wakiendelea na mazoezi, huku mtu aliyetambulika kwa jina moja la Kingwele akiwa mstari wa mbele kutoa mafunzo hayo.

Majirani waliokuwapo katika jengo hilo, waliliambia MTANZANIA kuwa mafunzo hayo yameanza pindi wabunge na wanachama wa upande wa Maalim Seif walipotangaza kuingia ofisi kuu Buguruni kwa madai ya kufanya usafi katika ofisi hizo.

KAULI YA POLISI

Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro, alipoulizwa na MTANZANIA kuhusu suala hilo, alisema bado hajapata barua rasmi inayoonyesha wabunge hao watafanya usafi Jumapili.

Hata hivyo, aliahidi kuwa leo atazungumza na waandishi wa habari kulitolea ufafanuzi suala hilo.

“Hatujapata barua rasmi, lakini kesho (leo) nitazungumza na waandishi wa habari kulitolea ufafanuzi suala hilo,” alisema Sirro.

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS

JIUNGE NA ST MARY'S INT'L SCHOOLS